RAIS MWINYI:JENGO JIPYA LA ZEC KUIMARISHA DEMOKRASIA ZANZIBAR.

 




Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Ujenzi wa Jengo jipya la Tume ya Uchaguzi  unalenga Kuiimarisha Mifumo ya   Kidemokrasia Nchini .

Rais Dk, Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Afisi Kuu ya Tume ya Uchaguzi  Maisara ,Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha Rais Mwinyi ameeleza kuwa Kukamilika kwa Jengo hilo  kutamaliźa  tatizo Sugu la Muda mrefu  lililoikabili Tume ya Uchaguzi (ZEC) la kutokuwa na eneo  Bora la kufanyia kazi zake.

Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa Uamuzi wa   kulifanya Jengo hilo kuwa Kituo kimoja cha Shughuli zote za Uchaguzi ( One Stop Centre) kutaongeza Ufanisi kwa Watendaji wa tume.

Halikadhalika , Rais Dk.Mwinyi ameipongeza Tume ya Uchaguzi na Wakala wa Majengo (ZBA) kwa kazi nzuri ya Kusimamia Ujenzi huo  kwa Viwango bora na kuihimiza Kampuni ya CRJE   ambao ndio Wakandarasi wa Ujenzi huo kumaliza kazi kwa Wakati.

Naye,  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa ZEC  Thabit Idarous Faina ameeleza kuwa Ujenzi huo utakamilika na kuanza kutumika kabla ya Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka huu.

Ujenzi wa Majengo Mawili yenye Ghorofa nne  Utagharimu kiasi cha Takriban Shilingi Bilioni 11.32 utakapokamilika Fedha zilizotolewa na Mfuko Mkuu wa Serikali, kwa sasa Ujenzi umekamilika kwa Asilimia 81 .

Amefafanua kuwa Majengo hayo Mawili moja litatumika kwa Shughuli za Afisi za Tume  na jengine  kwa ajili ya Huduma za Shughuli za Uchaguzi.





















Post a Comment

0 Comments