KABLA YA BONDIA MGAYA KUZIKWA FEDHA RAMBIRAMBI ZAZUA MINONG'ONO KWA KASEBA, CHEKA
Kuelekea mazishi ya bondia Hassan Mgaya yatakayofanyika leo katika maeneo ya Jeti lumo jijini Dar es salaam uongozi wa chama cha mabondia waja na mitazamo tofautu kuhusu fedha za rambi rambi.
Marehemu Mgaya atazikwa leo saa saba mchana jijini Dar es salaam lakini chama cha mabondia kinachoratibu suala la mazishi hayo kimeonekana kukinzana kihusu kuwekwa mchanganuo wa fedha za za rambirambi ambazo huchangishwa na wadau mbalimbali kwaajili ya kukabidhiwa kwa wafiwa.
Akiongea katika mahojiano niliyofanya nae mwenyekiti wa chama cha mabondia nchini Tanzania, Japhet Kaseba amesema kumekua na sintofahamu ya pesa zinazopelekwa kwa wafiwa bila wadau kujua imepatikana kiasi kilichopatikana kwenye michango yote na kile kilichowasilishwa kwa wahusika.
"Watu wameanzisha utaratibu wa kuchangisha pesa kwenye magroup ya whatsap wanachanganya na pesa ya chama cha mabondia ambayo ni laki mbili inayotolewa kwa familia ya bondia husika na pesa ya TPBRC na kupeleka kwa mfiwa au bondia aliyepata tatizo bila kusema kiasi gani kilichopatikana na mwisho wa siku watu kuanza kuhisi labda pesa zingine zimeliwa.
"Pesa inapokabidhiwa kwa wafiwa inatakiwa itamkwe palepale sisi chama cha mabondia tumetoa kiasi gani na michango ya magroup imepatikana kiasi gani na TPBRC imetoa kiasi gani kwasababu hizi pesa ni mali ya mabondia na sio mali ya viongozi wa chama na itasaidia kuweka kumbukumbuku sawa ya mapato na matumizi ya chama chetu,"amesema Kaseba.
Kwa upande wake mweka hazina wa chama hiko, Cosmas Cheka amesema pesa ya mchango wa msiba si busara kuitangaza kwaajili ya kulinda faragha ya tukio la msiba.
"Pesa ya mchango wa msiba haitangazwagi na haina ufahari kutangaza na wakitaka majukumu yangu wachukue mimi nishachoka,"amesema Cheka.
Pia Cheka ameweka wazi anavyotumia muda wake wa ziada na nguvu yake binafsi kwaajili ya kufanikisha masuala hayo yanayowahusu mabondia.
"Nashindwa kupumzika kwaajili ya kushugulikia masuala ya mabondia na muda mwingine natoa hadi pesa yangu mfukoni ili mambo yaende,"amesema Cheka.
0 Comments