TANZANIA YAINGIA TATU BORA KWENYE MASUMBWI

 


Na mwandishi wetu

Tanzania imeshika nafasi ya tatu katika nchi zinazofanya vizuri kwenye ubora wa ngumi za kulipwa barani Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa ya viwango vilivyotolewa January 2025 chini ya shirikisho la mkanda wa ABU chini ya mwenyekiti wake Houcine Houichi nchi ya kwanza ni Afrika Kusini ya pili Nigeria na ya tatu ni Tanzania.

Taarifa hiyo imeonesha kwenye viwango hivyo nchi ya Afrika Kusini imeongoza kwa kuingiza mabondia wengi kwenye vipengele mbalimbali vya orodha hiyo pia imeingiza idadi kubwa ya mabondia kuliko Nigeria na Tanzania ambazo zimepisha kidogo.

Nchi ya Afrika Kusini imekua ya kwanza imefanikiwa kuingiza mabondia takribani 36 kwenye jumla vipengele 16 kati ya vipengele 18 vya mdaraja ya uzito tofauti.

Nigeria imekua nchi ya pili kwa ubora baada ya kuingiza mabondia 18 kwenye vingele  13 vya madaraja ya uzito tofauti.

Na kwa upande wa Tanzania imekua ya tatu baada ya kuingiza mabondia takribani 18 kwenye vipengele 11 kati ya vipengele vyote 18 vya madaraja tofauti ya kila uzito.

Post a Comment

0 Comments