Na mwandishi wetu
Mkuu wa wilaya ya Tanga Mhe Japhari Kubecha Ameshiriki Kusherehekea Sikukuu ya Eid Pamoja na Watoto Wenye Uhitaji ,Sherehe Hizo Ziliandaliwa na Taasisi ya Islamic Help na Kufanya katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kombezi .
Aidha katika Sherehe Hizo za Eid Zilijumuisha Takribani watoto 820 Huku Watoto 450 Wakitokea Wilaya ya Handeni na 370 Wakitokea Wilaya ya Tanga Mjini .
Mkuu Wilaya Aliwashukuru Islamic Help kwa namna wanavyojitoa kuhudumia Jamii kama Wadau muhimu wa maendeleo katika nyanja za Kiuchumi , pia Akaendelea Kukazia kwa Kuelekeza Utokomezaji wa Swala la Ukatili kwa Watoto ili Kusaidia Waweze kutimiza ndoto zao .
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Akaendelea Kutoa Wito kwa Wazazi Kuhakikisha Wanawalinda Watoto Kwenye Kipindi Hiki cha Sikukuu za Eid ili Kuepuka Changamoto Mbalimbali ambazo Zitajitokeza , na Kuwasisitiza Maafisa Ustawi ,Watendaji wa kata na Mitaa na Wenyeviti Kuhakikisha Wanaendeleza Kampeni za Kutokomeza Ukatili ndani ya Wilaya ya Tanga .
#TANGA YETU ,LANGO LA UCHUMI WA AFRIKA*
0 Comments