RAIS MWINYI:SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUKUZA UTALII ENDELEVU.

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Sekta Binafsi Ina Mchango Mkubwa katika Kukuza Sekta ya Utalii hapa nchini katika Nyanja tofauti na kusisitiza Serikali  Kuendelea kushirikiana na Sekta binafsi Ili kuwa na Utalii Endelevu.

Rais Dkt,Mwinyi amesema  hayo alipoifunga Ziara Maalumu ya Mabalozi (Safari Diplomatic Tour) wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini iliolenga kuutangaza Utalii wa Tanzania na diplomasia  ya Kiuchumi katika Nchi zao iliofanyika  Hoteli ya  Kwanza Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 14 Aprili 2025.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua Madhubuti za Kuimarisha Sekta ya Utalii Ili kuwa Endelevu na kuifanya Zanzibar kuwa Kituo Muhimu cha Utalii kinachotambulika  na kuvutia Ulimwenguni.

Amefahamisha kuwa Utalii ni Sekta Muhimu na nguzo ya Uchumi wa Zanzibar ambayo mbali na Kukuza Uchumi Sekta Hiyo Inawaunganisha Watu wa Mataifa mbalimbali Ulimwenguni.

Rais Dkt, Mwinyi amesema Serikali  imechukua Juhudi  kubwa za Uimarishaji wa Viwanja vya Ndege kwa lengo la kutoa huduma Bora kwa Watalii ,Upanuzi wa Miundombinu ya Barabara  pamoja na Huduma za Afya,Umeme na Upatikanaji wa Maji ni hatua Muhimu za kufanikisha  kuwa na Utalii unaovutia na  Endelevu.

Amebainisha kuwa kuchukua hatua Hizo Nchi imekuwa ikipokea Idadi kubwa ya Watalii kila Mwaka wanaofikia takribani Milioni mbili na Kuiunganisha Zanzibar na Mashirika ya Kimataifa ya Ndege 34 yanayoleta Watalii hapa nchini

Aidha Rais Dkt, Mwinyi ameielezea Filamu ya Royal Tour ya Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan na Ziara yake kuwa ni nyenzo Muhimu zilivyovitangaza Vivutio vya Utalii wa Tanzania kwa Mafanikio Ulimwenguni.

Rais Dkt.Mwinyi amesema mikakati ya Uwekezaji imewezesha kupokea Watalii 548,503 Mwaka 2022 na Mwaka 2023 imepokea Wageni 736,755 na kutunukiwa Tuzo  ya World Travel Award kwa kuwa Kituo kinachoongoza kwa Matamasha na Mikusanyiko ya  kimataifa .

Akizungumzia Safari Diplomatic Tour amesema ni hatua Muhimu ya Ushirikiano Miongoni mwa Mataifa kupitia Sekta ya Utalii na  kuwaomba Mabalo











Post a Comment

0 Comments