WASIRA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 53 YA KIFO CHA KARUME

 



Na mwandishi wetu

Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM (Bara) Ndg. Stephen Wasira leo Aprili 7, 2025 ameshiriki Maadhimisho ya  Kumbukumbu ya Miaka 53 ya kifo cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amani Karume kwenye Afisi Kuu ya CCM Kisiwandua  Zanzibar.

Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, Mjane wa Hayati Karume, Mama Futuma Karume, Watoto ya Hayati Karume, Amani Abedi Karume na Balozi, Ali Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein.







Post a Comment

0 Comments