Na mwandishi wetu
Ni Kutokana na Uwepo Tume huru na mabadiliko makubwa ya sheria za uchaguzi
Atakayeshinda kwa haki Atangazwe mahindi
DAR ES SALAAM:Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemesema kutokana na mabadiliko yaliyofanyika katika sheria ya uchaguzi, uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu utakuwa huru na wa haki.
Pia amewakumbusha wale wanaodhani uchaguzi huru na haki ni pale tu chama tawala kinaposhindwa uchaguzi hiyo ni fikra potofu : Demokrasia ya kweli ni chama kinachoshinda kwa haki kitangazwe mshindi
Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla amesema hayo leo Aprili 30,2025 wakati akizungumza na wananchi katika Uwanja wa Madenge Wilaya ya Temeke Dar es salaam, akihitimisha ziara yake ya siku tatu katika mkoa huo.
Makalla ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Dar es salaam amekuwa na ziara fupi iliyofanyika katika Wilaya tatu ya Ubungo, Kinondoni na Temeke akifanya mikutano ya hadhara kuzungumza na wananchi wa wilaya.
Akizungumza na wananchi wa Temeke Makalla amesema katika uchaguzi Mkuu Tume Huru ya Uchaguzi itatenda haki na CCM wanataka kweli watende haki na kuwataka watu kuachana na desturi wanayojiwekea kuwa chama tawala kikishinda uchaguzi si demokrasia.
“Kwa Tume hii ilivyohuru itatenda haki na sisi tunataka itende haki, maana kuna tabia imejengwa kwamba chama tawala kinaposhindwa ndiyo demokrasia ya kweli wakubali pia chama tawala kinaposhinda ni demokrasia ya kweli,” amesema Makalla.
Pia Makalla amesema CCM haijiweki madarakani yenyewe bali inawekwa madarakani na wannachi kupitia sanduku la wapiga kura na hadi wanaaminika ni kutokana na rekodi yao ya utendaji wa kazi mzuri na kuwapelekea wananchi maendeleo wanayoyahitaji.
Makalla amesema hitaji kubwa la wananchi ni maendeleo na ndiyo sababu inayowafanya wananchi wanaendelea kuiamini CCM katika chaguzi nyingi zinazofanyika.
0 Comments