MBUNGE WA VITI MAALUM AOMBA RIDHAA KUGOMBEA JIMBO LA MBOGWE




Mbogwe, Geita – Juni 29, 2025


Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Geita, Mheshimiwa Rose Vicent Busiga, leo Juni 29, 2025, amechukua na kurejesha rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kupitishwa kugombea Ubunge wa Jimbo la Mbogwe katika uchaguzi mkuu Wa mwaka huu 2025.

Mheshimiwa Busiga aliwasili mapema leo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Mbogwe na tayari amekamilisha Hatua hiyo ya kuchukua na kurejesha.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi ya Ubunge kupitia CCM linaendelea nchi nzima, ambapo wanachama mbalimbali wa chama hicho tawala wanaendelea kujitokeza kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo yao.

Hatua hii ya Mhe. Busiga ni ishara ya kuendeleza dhamira yake ya kulitumikia Taifa na wananchi wa Mkoa wa Geita kwa moyo wa uzalendo na uaminifu aliouonesha katika kipindi chake cha awali akiwa Mbunge wa Viti Maalum.

Post a Comment

0 Comments