CCM NI CHAMA BORA CHENYE MISINGI IMARA YA KIDEMOKRASIA NA MAENDELEO YA VIJANA

 



Na mwandishi wetu

Tangu kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari 1977 kwa muungano wa TANU na ASP, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimejidhihirisha kuwa ni chama kinachoongoza kwa uwezo wa kutoa dira ya maendeleo, kulinda amani na mshikamano wa kitaifa na kutambua kikamilifu nafasi ya vijana katika ujenzi wa Taifa. Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, Chama kinaelekeza kuwa moja ya malengo yake makuu ni “kukuza na kudumisha mshikamano wa kitaifa kwa njia ya demokrasia na usawa, bila kujali umri, jinsia wala kabila.”


1. CCM NA HISTORIA YA KUWAJENGA VIJANA KUWA VIONGOZI WA TAIFA

Katika historia ya harakati za kisiasa nchini, vijana wamekuwa mstari wa mbele Mwalimu Julius Nyerere alishiriki kuanzishwa TANU akiwa na umri wa miaka 32 na Mzee Rashid Kawawa akiwa na miaka 28 ,na uhuru wa Tanganyika umepatikana mwaka 1961 Mwalimu Nyerere akiwa na miaka 37. Hii ni ishara tosha kuwa msingi wa mapambano ya uhuru na maendeleo ya taifa ulijengwa na vijana. CCM imerithi urithi huu kwa dhati na kuendeleza mtazamo huo kwa vitendo tunaona kwa macho yetu kuwa CCM ni chama kinachowapa fursa kubwa vijana na kinatambua mchango wa vijana.

Kwa mfano, kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), chama kimekuwa na chombo maalumu kwa ajili ya kuwaandaa vijana kitaaluma, kiitikadi na kiuongozi. Katiba ya CCM imetambua Jumuiya ya UVCCM kama mojawapo ya mihimili mitatu ya chama katika kukuza uongozi na ushiriki wa makundi maalum. Miongozo ya chama inasisitiza kuwa nafasi ya vijana si ya huruma bali ni haki na wajibu. Vijana wanashiriki katika vikao vyote vya maamuzi kuanzia ngazi ya tawi,shina,kata,wilaya,mkoa hadi taifa.mfano mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi katika ngazi yeyote ni mjumbe wa kikao cha kamati ya siasa,kikao cha halmashauri kuu kwa ngazi husika, hii inamaana vijana wanashiriki katika maamzui yote katika jamii.

2. ILANI YA CCM 2020-2025 NA 2025-2030 NI USHAHIDI WA KUJALI VIJANA KWA VITENDO

Katika Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020-2025 na ile ya 2025-2030, CCM imeweka bayana mikakati thabiti ya kuwawezesha vijana. Baadhi ya hatua zilizotekelezwa na Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni pamoja na:-

  • Ajira kwa Vijana: Zaidi ya ajira 8,084,203 zilitengenezwa kati ya 2020 hadi 2024, ambapo zaidi ya 7 milioni ni ajira zisizo rasmi. Katika Ilani ya 2025-2030, CCM inalenga kuongeza kasi ya ajira kwa wastani wa asilimia 7 ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka.
  • Mikopo kwa Vijana: Kupitia mapato ya Halmashauri, shilingi bilioni 96.3 zilitolewa kwa vijana 8,242 kati ya 2020 hadi 2024. Hii ni pamoja na mikopo yenye masharti nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
  • Elimu na Mikopo ya Elimu ya Juu: Idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu walionufaika na mikopo iliongezeka kutoka 142,170 mwaka 2020 hadi 245,799 mwaka 2024. Wanafunzi wa stashahada 9,959 walipata mikopo katika fani zenye kipaumbele.
  • Samia Scholarship: Mpango huu umefadhili wanafunzi 3,696 katika masomo ya sayansi, tiba, na uhandisi. Ni mpango unaodhihirisha jinsi Serikali ya CCM inavyowekeza katika rasilimali watu ya vijana.
  • Elimu bila malipo kuanzia awali hadi kidato ha sita imekuwa ikitolewa ikiwapa fursa Watoto wa kitanzania na vijana kupata elimu bila kikwazo chochote. CCM iendelea kuwa na Imani kubwa sana vijana tumeshuhudia ziadi ya salimia 50 vijana waeteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi kama wakuu wa wilya,wakurugenzi wa halmashauri, wakuuw mikoa, mawaziri, wabunge .Chama cha mapinduzi kinatambua mchango wa vijana katika maendeleo ya taifa. 3. HATUA ZA UCHUKUAJI FOMU NA FURSA ZA KISIASA KWA VIJANA

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM na kanuni zake, vijana wana nafasi zote sawa za kugombea nafasi kuanzia ngazi ya serikali za mitaa , udiwani hadi ubunge, ili mradi tu wamekidhi vigezo vya kikatiba. CCM imefanya maboresho ya kanuni mnamo Machi 2025 yaliyoongeza demokrasia na ushiriki wa vijana Wigo wa Kura za Maoni umeongezwa,  Vijana wengi zaidi sasa wanashiriki kupiga na kupigiwa kura., Ukomo wa Viti Maalum kwa Wanawake umewekwa: Hii imefungua nafasi zaidi kwa vijana wanawake kugombea majimbo au kata.

Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 2024, zaidi ya asilimia 60 ya waliochaguliwa katika maeneo mengi walikuwa vijana. Huu ni ushahidi kuwa vijana wa CCM wanaungwa mkono na wananchi na chama chao. Mfano mkoa wa Kigoma asilimia 95 walioshinda uchaguzi wa serikali za mitaa walikuwa ni vijana

 

4. UTEKELEZAJI WA ILANI NA CCM KINAVYOGUSA MAISHA YA VIJANA NA WANANCHI KWA UJUMLA

Kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya 2025-2030:

  • Ajira na Uwezeshaji Kiuchumi: Serikali itaendelea kutoa mikopo yenye masharti nafuu, kuimarisha huduma jumuishi za kifedha, na kuboresha mazingira ya biashara kwa vijana.
  • Maendeleo ya Sayansi na TEHAMA: CCM inalenga kufundisha vijana ujuzi wa TEHAMA, kuongeza matumizi ya teknolojia katika ajira, biashara na ubunifu.
  • Michezo na Sanaa: Serikali ya CCM inakuza sekta ya sanaa na michezo kuwa fursa ya ajira kwa vijana. Dkt. Samia alianzisha Tamasha la Sanaa la Samia (Samia Youth Art Fund) na kuwekeza katika miundombinu ya michezo.
  • Ruzuku ya Elimu na Elimu Bila Malipo: Shilingi trilioni 1.3 zilitumika kuendesha elimu bila ada kutoka awali hadi sekondari kati ya 2020-2024

Post a Comment

0 Comments