Tanzania Yazishukuru Nchi za Afrika Katika Uhifadhi

 



Na mwandishi wetu

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, leo Julai 12, 2025, ameshiriki kikao maalum cha kundi la Afrika (Africa Group) pembezoni mwa Mkutano wa 47 wa Kamati ya Urithi wa Dunia ya Unesco unaoendelea mjini Paris, Ufaransa.

Vikao vya Kundi la Afrika hufanyika ili kujadili maeneo ya Urithi wa Dunia ya Afrika kwa lengo la kijipanga namna ya kushirikiana wakati wa majadiliano ya pamoja na mabara mengine ili kulinda maslahi ya Bara hilo. 

Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Ali J. Mwadini pamoja na wataalam kutoka Tanzania ambapo Dkt. Abbasi na Balozi Mwadini walipata fursa ya kuwasilisha salaam za Tanzania na kushukuru Kamati hiyo na nchi za Afrika kwa namna zinavyofanyakazi kuzisaidia nchi za Afrika kulinda maslahi yao.

Tayari ripoti za hali ya uhifadhi kwa maeneo ya Tanzania yaliyoko kwenye orodha ya urithi wa dunia ambayo yalitakiwa kuleta taarifa za hali ya uhifadhi mwaka huu ya Ngorongoro, Selous na Kilwa yameshapitishwa na kuidhinishwa na vikao vya Unesco.




Post a Comment

0 Comments