JUMLA YA WANAFUNZI 62,950 WAMEWASILISHA MAOMBI HESLB,DKT KIWIA AFUNGUKA HAYA.

 


Na mwandishi wetu


BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema jumla ya waombaji 62,950 wawewasilisha maombi ya mkopo wa masomo ya mwaka 2025/2026 kati ya waombaji 107,059 ambao wamesajili kupitia mfumo wa maombi ya mikopo wa HESLB.

Hayo yamebainishwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa (HESLB),Dkt.Bill Kiwia,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia mwenendo wa Uombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2025/2026.

Dkt Kiwia amesema maombi hayo yanahusisha waombaji wa mikopo ya stashahada,shahada ya awali,stashahada ya juu ya mafunzo ya sheria kwa vitendo,shahada za uzamili na uzamivu.

"Idadi hii inaonesha mwitikio mzuri kutoka kwa wanafunzi wenye sifa wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu na vyuo vya kati nchini"amesema Dkt Kiwia.

Mbali na waombaji hao ,amesema zaidi ya wanafunzi elfu moja watanufaika na ufadhili wa Samia Scholarship kwa mwaka 2025/2026 ambapo hadi kufikia leo wanafunzi 603 wamekamilisha na kuwasilisha maombi kati ya wanafunzi 889 ambao wamejaza fomu

Dkt Kiwia,amesema Serikali kwa 2025/2026 imetenga Bilioni 916.5 inatarajiwa kunufaisha wanafunzi 252,773 wakiwemo wanafunzi 88,320 wa mwaka kwanza na wengine 164,453 wanaendelea na masomo.

Hata hivyo,Dkt Kiwia amewata  wanafunzi ambao hawajaomba wawaendelee kujaza,kukamilisha na kuwasilisha maombi ndani ya muda uliotolewa ili kuepuka msongamano wa tarehe ya mwisho 31 Agosti,2025 na hawataongeza muda.

Post a Comment

0 Comments