DKT. MWINYI: SERIKALI IJAYO KUWEKA KIPAUMBELE KWENYE CHAKULA NA MAFUTA

 


Zanzibar, Septemba 12, 2025 –

Mgombea wa Urais kupitia CCM Zanzibar, ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ijayo itaweka kipaumbele katika sekta ya chakula na mafuta ili kuhakikisha upatikanaji wa uhakika na kudhibiti mfumuko wa bei.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Golden Tulip, Airport, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dkt. Mwinyi alieleza kuwa hatua zitakazochukuliwa ni pamoja na:

👉 Ujenzi wa maghala ya kuhifadhia chakula kwa ajili ya kuhakikisha akiba ya kutosha ya chakula nchini.

👉 Ununuzi wa mazao ya wakulima wakati wa mavuno, kutoa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu.

👉 Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na kuhakikisha soko la uhakika kwa mazao ya wakulima.

👉 Ujenzi wa matangi makubwa ya mafuta katika maeneo mbalimbali nchini ili kudhibiti athari za mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia.

Ukuaji wa Uchumi

Dkt. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikisha ukuaji wa uchumi kutoka asilimia 4 mwaka 2020 hadi asilimia 7 mwaka 2024. Pia imeongeza mishahara, pensheni na posho ili kuboresha maisha ya wananchi.

Vipaumbele Vingine

Aidha, alibainisha kuwa Serikali itaimarisha huduma za bandari, utafutaji na uchimbaji mafuta na gesi, pamoja na kuongeza thamani ya zao la mwani ambalo ni tegemeo la akinamama wengi Zanzibar.

Wito wa Amani

Akihitimisha hotuba yake, Dkt. Mwinyi alisisitiza umuhimu wa kudumisha amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Pia aliahidi kampeni safi na za kistaarabu kupitia CCM.










#Zanzibar2025 🟢

#UongoziUnaoachaAlama

#DktMwinyi

Post a Comment

0 Comments