Na mwandishi wetu
Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ijayo itaongeza bajeti na kuwekeza zaidi katika kilimo na ufugaji ili wananchi wanufaike kiuchumi.
✅ Wakulima watapatiwa pembejeo, mbegu bora, mbolea na masoko ya bidhaa zao kwa wakati.
✅ Wafugaji watawezeshwa mikopo isiyo na riba na kuunganishwa na masoko ya uhakika.
✅ Mikopo midogo itawasaidia wananchi kuendeleza shughuli zao za uzalishaji.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Michezo Uzini, Wilaya ya Kati , Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 16 Septemba 2025.
Akihitimisha, amewataka wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, ili kuendelea kuleta maendeleo kwa Zanzibar.
0 Comments