Na mwandishi wetu
Picha hii inaonesha uhalisia wa uongozi wenye kuzingatia mshikamano na mashauriano kati ya viongozi wakuu wa taifa, hasa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, na vijana kupitia kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Komredi Mohamed Kawaida.
Huu ni uthibitisho kwamba vijana hawapuuzwi; wanashirikishwa kikamilifu, wanasikilizwa na kuthaminiwa katika safari ya kuijenga Tanzania mpya yenye mshikamano na ushirikiano.
Ujumbe huu unazungumza moja kwa moja na mioyo ya vijana wote kupitia kwa Mwenyekiti wetu na Sauti ya Vijana, Komredi Kawaida. Ni mwito wa mshikamano na matumaini kwamba kizazi kipya kina nafasi kubwa ya kushirikiana na viongozi katika kuleta mabadiliko chanya.
Hii ndiyo nguzo ya taifa lenye mshikamano wa kijamii, mshirikiano wa kisiasa, na maono ya maendeleo endelevu.
0 Comments