Na mwandishi wetu
Kupitia sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, vijana ndio wengi kuliko makundi mengine, na hivyo wanakwenda kuwa kinara katika kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata kura za kishindo kuanzia ngazi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wabunge, na madiwani wanaotokana na CCM.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndugu Rehema Sombi Omary (MNEC) wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais uliofanyika katika Uwanja wa Bombadia, Mkoani Singida, wakati Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipofika mkoani humo.
> 💬 "Yote haya ni kwa sababu Dkt. Samia Suluhu Hassan umeendelea kutugusa vijana katika nyanja mbalimbali na tunaona kwa macho kila mradi, ajira au fursa kijana yupo ndani." – Ndugu Rehema Sombi Omary
Sombi ameendelea kwa kusema kuwa itakapofika tarehe 29 Oktoba, vijana watahakikisha Dkt. Samia anapata kura za kishindo, ikithibitisha mshikamano wa vijana na sera za maendeleo zinazolenga kundi hili.
Jiunge Na Wote Vijana 👇
✅ Wacha sauti yetu isikike!
📢 SHARE habari hii na marafiki wako ili kila kijana ajue umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika uchaguzi.
#OktobaTunatiki
#FyuchaBilaStresi
#KaziNaUtuTunasongaMbele
0 Comments