Mbeto: Amani na Umoja Funguo za Milango ya Maendeleo

 


Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitasita kuzihimiza Serikali zake kuendelea kuongeza mkazo katika kuhakikisha hakuna mtu au kikundi chochote kinachoweza kuvuruga amani na umoja wa kitaifa.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamisi Mbeto Khamis, amebainisha kuwa siri ya mafanikio na maendeleo ya haraka katika Awamu ya Nane Zanzibar ni ustawi wa amani, mshikamano na utulivu.

"Nchi ikiwa katika mazingira ya umoja, milango ya neema ya maendeleo hufunguka,” alisema Mbeto.

Mbeto alieleza kuwa pale amani inapokosekana, serikali haiwezi kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo madaraja, maji, shule, barabara, bandari, viwanja vya ndege, michezo na masoko.

Aidha, alisema CCM imeendelea kuzielekeza Serikali zake kuhakikisha hakuna mtu anayechekewa endapo atathubutu kuvuruga tunu za amani na mshikamano wa taifa.

Katika maelezo yake, Mbeto alitaja pia kuwa mafanikio ya ujenzi wa miradi ya maendeleo yamechochewa na kasi ya ukusanyaji wa

Mbeto aliongeza kuwa hivi sasa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepata kibali cha uaminifu wa kukopa katika taasisi mbalimbali za fedha na benki.

Vilevile, aliwaeleza wananchi kuwa CCM inaingia katika mbio za Uchaguzi Mkuu kwa matumaini makubwa ya ushindi kutokana na mgombea wake, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye alimtaja kama kiongozi mchapakazi, muaminifu na mzalendo.

“Ushindi wa ngwe ya pili utazidi kupanua wigo wa maendeleo yatakayowashangaza wengi katika ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Mbeto.

Post a Comment

0 Comments