NCHIMBI AAGANA NA WANA KAGERA, SASA ZAMU YA RUKWA

 



Bukoba, Kagera

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, ameagana na wananchi pamoja na viongozi wa Chama na Serikali katika Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo, Jumatatu Septemba 8, 2025, baada ya kumaliza ziara yake ya kampeni mkoani Kagera.

Katika ziara hiyo, Dkt. Nchimbi alipata fursa ya kuzungumza na wananchi katika mikutano mbalimbali ya kampeni, akiwataka kuendelea kukiamini na kukipigia kura Chama Cha Mapinduzi ambacho kimeonesha dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo.

Wananchi waliokuwa uwanjani walimpongeza Dkt. Nchimbi kwa juhudi zake na kumpa mwitikio mkubwa. Mmoja wa wananchi, Bi. Zainabu Mwakaje, alisema:
"Tumempa Dkt. Nchimbi sapoti yetu kwa sababu tunaona anajali maendeleo ya kila mmoja wetu. Tunaiamini CCM itatupeleka mbali."

Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya mkoa huo, Jonas Mjema, alisema:
"Tunafurahia kuona viongozi wanapokaa na wananchi, wanatuuliza tunachohitaji. Hii ni matumaini mapya kwa vijana wa Kagera."

Baada ya kuhitimisha kampeni zake mkoani humo, Dkt. Nchimbi sasa anaelekea mkoani Rukwa kwa ajili ya kuendelea na mikutano ya kampeni, akihimiza wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika mikutano na pia kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.



Post a Comment

0 Comments