Na Mwandishi Wetu
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema kuwa CCM haina ugomvi na aliyekuwa Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, kwa kuwa chama kikubwa hakiwezi kugombana na mtu binafsi.
Wasira aliyasema hayo jana, wilayani Kisesa mkoani Simiyu, alipokutana na viongozi na wanachama wa CCM katika kikao cha ndani chenye lengo la kuvunja makundi na kuwaunganisha wana-CCM ili kujenga mshikamo wa pamoja kuelekea ushindi wa mgombea urais, Dk. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wagombea ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu ujao.
“CCM ni chama kikubwa sana katika Afrika. Wengine huja kutuuliza mnaendeleaje, sasa fikiria wasikie eti Chama kinagombana na Mpina. Hapana, sisi hatuna ugomvi na Mpina,” alisema Wasira.
Aidha, Wasira aliwataka ndugu na familia ya Mpina kumlea kiakili, hasa baada ya kukosa nafasi ya kugombea urais, ili aendelee kuwa mwanakijiji mwema wa Mwandoya.
"Kazi ya kumlea itakuwa ya familia na majirani zake kwa sababu urais hawezi kupata, tunajua. Pia hatumwambii ukikosa urudi, ni hiyari yake. Ila akirudi tutampokea, lakini hatumwambii lazima arudi. Si lazima awe rais, anaweza tu kuwa mwanachama wa kawaida wa chama chake kipya,” aliongeza.
Wasira pia alibainisha kuwa changamoto kubwa kwa Mpina ni ukweli kwamba katika eneo la Kisesa, chama chake kipya hakina wanachama wengi, isipokuwa yeye mwenyewe.
“Kazi ya kumlea itakuwa ya familia na majirani zake kwa sababu urais hawezi kupata, tunajua. Pia hatumwambii ukikosa urudi, ni hiyari yake. Ila akirudi tutampokea, lakini hatumwambii lazima arudi. Si lazima awe rais, anaweza tu kuwa mwanachama
0 Comments