TANESCO KIGAMBONI YAENDELEA KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME

 




Na mwandishi wetu

Septemba 03, 2025

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kigamboni limefanikisha kukamilisha mradi wa umeme katika Mtaa wa Ngoma Mapinduzi, Uwalani kwa kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo.

Mradi huo umehusisha usimikaji wa transfoma mbili zenye uwezo wa 100 kVA kila moja, hatua itakayoongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wakazi wa eneo husika.

Hatua hii ni sehemu ya mikakati ya TANESCO Kigamboni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ya umeme na kuondokana na changamoto za upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya pembezoni.





Post a Comment

0 Comments