WANANCHI WA JIMBO LA KWELA, SUMBAWANGA VIJIJINI

 



Na Mwandishi Wetu, Rukwa

Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, leo Jumatatu Septemba 8, 2025, amewahutubia wananchi wa Jimbo la Kwela katika Uwanja wa Laela A, Sumbawanga Vijijini, katika mkutano mdogo wa hadhara wa kampeni.

Katika hotuba yake, Dkt. Nchimbi aliwaeleza wananchi dhamira ya CCM kuendelea kuwaletea maendeleo endelevu kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi, huku akisisitiza mshikamano wa kitaifa na mshikamanisho wa sera za chama hicho.

Baada ya hotuba hiyo, Dkt. Nchimbi alitumia nafasi hiyo kuwanadi wagombea wa nafasi za Ubunge katika Mkoa wa Rukwa, akiwemo Mbunge wa Jimbo la Kwela, Deus Clement Sangu, pamoja na madiwani wanaogombea kupitia tiketi ya CCM.

Aidha, amewataka wananchi wa Rukwa kuendelea kuiamini CCM kwa maendeleo ya kweli, akibainisha kuwa chama hicho ndicho chenye uwezo na uzoefu wa kutatua changamoto zinazowakabili Watanzania.

Dkt. Nchimbi ameingia mkoani Rukwa leo kuendeleza mikutano yake ya kampeni ya kusaka kura za kishindo kwa CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika oktaba 29,2025.






Post a Comment

0 Comments