Na mwandishi wetu
Zanzibar, Septemba 12, 2025 – Wasanii mbalimbali wa muziki na sanaa za maonesho wamejitokeza na kutumbuiza katika tukio kubwa la uzinduzi wa kampeni za urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), linalofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Uzinduzi huu umehudhuriwa na maelfu ya wananchi, wanachama wa CCM na wageni mashuhuri, huku wasanii wakitoa burudani ya aina mbalimbali ikiwemo muziki wa kizazi kipya, taarab, na ngoma za asili. Burudani hizo zimeongeza hamasa na shangwe kwa umati uliokusanyika kushuhudia tukio hilo la kihistoria.
Aidha, tukio hili linaashiria mwanzo wa safari ya kampeni za CCM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo wananchi wanaonesha mshikamano mkubwa kwa chama chao na mgombea wao wa urais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Kwa ujumla, burudani za wasanii zimekuwa sehemu muhimu ya kuongeza shauku na hamasa, huku zikionesha mshikamanano wa kijamii na kisiasa kuelekea ushindi wa CCM.
✅ #ZanzibarMpya
✅ #UongoziUnaoachaAlama
✅ #OktobaTunatiki
0 Comments