JWTZ,SHULE YA MAKONGO WAMEHADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO KWA KUWAKUMBUKA WATOTO NJITI

 


NA MWANDISHI WETU 

Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi namba 302 KV ADM COY na shule ya Makongo wamehadhimisha miaka 59 ya Muungano ya Tanzania kwa kuwakumbuka watoto Njiti, Tukio hilo limefanyika leo tarehe 26 April 2023 katika Hospital ya Mwananyamala Kinondoni Jijini Dar es salaam.


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliundwa tarehe 26 April 1964 ikiwa ni Muungano ya mataifa mawili huru ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar ambayo yaliingia mkataba wa Muungano ya kuunda Dola ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkataba huu ilisaniwa na aliyekuwa Rais ya Jamhuri ya Tanganyika Hayati Mwl. Julius Nyerere na aliyekuwa Rais wa Zanzibar Hayati Abeid Karume, Hiyo kila ifakapo 26 April Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanahadhimisha siku hiyo ikiwa ni kusherekea na kuwaenzi waasisi wa Muungano huu.


Jeshi la ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni Jeshi liliamzishwa 01 September 1964 likiwa na lengo la kulinda uhuru nchi na mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, majukumu mojawapo ya JWTZ ni kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa hivyo JWTZ wanasherekea siku ya Muungano kwa kushirikiana na taasisi yake ya shule ya makongo imewatembelea watoto Njiti kwa kuwapatia maji, paperc na sabuni ikiwa ni moja ya majukumu yao na Utamaduni wao kila ifakapo 26 April. 


Shule ya Sekondari Makongo ni taasisi ya elimu inayomilikiwa na Jeshi la ulinzi wa wananchi Tanzania (JWTZ) iko chini ya kikosi namba 302 KV ADM COY, Makongo ni taasisi elimu inayotoa huduma ya elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita, elimu na mafunzo ufundi na elimu ya kurudia mitihani ya kidato cha nne(Pre form five), Akiongea na waandishi wa habari mara kukabidhi maji, paperc na sabuni Kaimu mkuu wa shu le ya Makongo amesema "Makongo ni shule inayomilikiwa na Jeshi la ulinzi ya wananchi wa Tanzania na tunatoa huduma mbalimbali ya kijamii kwanza kabisa tunatoa elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha sita, tunatoa elimu ya veta kwa maana ya mafunzo ya ufundi wa magari, ufundi wa umeme wa majumbani.... Tunatoa huduma ya elimu ya wanarodia mtihani wa kidato cha nne kwa maana Pre form five"


" Serikali yetu leo inahadhimisha miaka 59 ya muungano na imetolewa kauli mbiu ya serikali inayosema kwamba umoja na mshikamano ndio nguzo imara wa maendeleo ya uchumi wetu.. Kwa sababu ya kauli mbiu hiyo ambayo imetolewa na serikali na kwa maelezo ya mkuu wa majeshi ya Ulinzi wa wananchi wa Tanzania Jenerali Jacob John Nkunda akaelekeza katika taasisi zake ambapo shule ni miongoni mwa hizo taasisi na taasisi yetu ilipewa jukumu la kuwaona watoto Njiti tuweze kuwapatia huduma kama ulivyoona tumeweza kuwaletea maji, paperc na wives na pia tumefanya usafi wa mazingira katika hospital hii"


Kwa upande mwingine Major Godliver Swai amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Hassan Suluhu" Kama tunavyoona Jitihada za Rais Dkt Samia  Suluhu Hassan katika kuboresha huduma mbalimbali za afya tukaona kama taasisi tuje tumsupport Dkt Samia Suluhu Hassan hakika tanaona kazi yake ni kazi nzuri inayoonekana kwa macho ongoji kuhadithiwa, tunampongeza sana mama, Hongera mama"


Pia Major Godliver ameshukuru uongozi wa hospital ya Mwananyamala kwa kuwa pokea na kushirikiana vizuri katika kusherekea miaka 59  ya Muungano. 

Naye Muuguzi kiongozi wa zamu Hospitali ya Mwananyamala Florence Uledi amesewashukuru Jeshi la ulinzi wa wananchi wa Tanzania kuwaletea watoto Njiti vifaa tiba kwani kupokelewa takribani ya watoto Njiti 60 waliozaliwa kwa siku ya leo. 


Njiti ni mtoto anayezaliwa kabla ya wiki 37,kikawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa wiki ya 37 mpaka wiki 42 na Dalili zake ni mtoto Njiti ni kupumua kusiko kawaida, viungo vyake havijakomaa na huwa na nywele mwilini. Hospital ya Mwananyamala ni hospitali ya rufaa ya wilaya(Mkoa) ya kinondoni inayotoa huduma ya umma inayohudumiwa wakazi takribani milion 2.2 wa mkoa wa Dar es salaam na viunga vya jirani hasa hasa wakazi wa kinondoni na ubungo, Huduma wanazotoa ni upasuaji, wagonjwa wa ndani, maabara, dharura pamoja na huduma ya Afya ya uzazi.




Upande wa mama aliyezaa mtoto Njiti Salah John Senyika  amewashukuru Jeshi la ulinzi Wananchi wa Tanzania kwa kuwaletea vifaa tiba hivyo kwani ilikuwa tatizo ambalo imetapata suluhisho. 





 


Post a Comment

0 Comments