UMMY MWALIMU AKEMEA MATUMIZI YA CHUMVI NYINGI,SUKARI NYINGI NA MAFUTA MENGI KATIKA CHAKULA NI CHANZO CHA KISUKARI



Na Mwandishi wetu 

WAZIRI wa wizara ya Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema mojawapo wa vyanzo vya saratani ni matumizi ya chumvi, sukari na mafuta mengi katika chakula ni chanzo cha magonjwa yasiyo ambukizi ikiwemo kisukari na saratani, Kauli imetoa leo Jumanne 25 April 2023 aliposhiriki chakula cha jioni na wataalam wa magonjwa yasiyo ambukizi iliyoandaliwa na kikundi cha Afrika mashariki cha kusoma saratani (East Africa diabetes study group) iliyofanyika katika hotel ya  white sand hotel mbezi Beach Jijini Dar es salaam.


Kikundi cha Ukanda Afrika mashariki  cha Kusoma kisukari (East Africa diabetes study group) ni kikundi cha wataalam wa ugonjwa wa kisukari na magonjwa yasiyo ambukizi katika Ukanda wa Afrika Mashariki kikundi hiki kinahusisha wataalam mbalimbali kutoka sekta ya afya ambacho ni kikundi cha madaktari bingwa wa magonjwa ya kisukari, Moyo, mishipa na magonjwa yasiyo ambukizi mojawapo ya kipaumbele ni  Kuzuia ugonjwa wa kisukari kwa kuendeleza watu binafsi na jamii yenye afya, hasa watoto; kukuza shughuli za mwili, kula afya na mazingira ambayo yanahimiza shughuli, hivyo kikundi hiki wankutana katika Kongamano la sita la vipindi na maonyesho ya kisayansi ambayo kongamano hili lina  kina, la taaluma nyingi na kitivo cha viongozi katika ugonjwa wa kisukari na Magonjwa mengine Yasiyo ya Kuambukiza ambayo huunganisha jumuiya ya wanasayansi na kuharakisha ugunduzi wa sayansi ya maisha. Wanawaleta pamoja wadau na viongozi wakuu zaidi ya 300 ili kujadili matarajio,vipaumbele na hatua za mabadiliko ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika Ukanda wa Afrika Mashariki, Kongamano hili limeanza leo Jumatano tarehe 26 April 2023 mpaka Jumamosi tarehe 29 April 2023, Jana Jioni Jumatano 25 April wameandaa chakula wakishiriki na wasaili wa kongamano hilo, wadau na serikali kupitia Wizara ya Afya. 



Kisukari ni ugonjwa yasiyo ambukizi  unao athiri selli za mwili,katika ugonjwa wa kisukari aina ya 2, seli za mwili haziathiriki na insulini jinsi ipasavyo. Insulini ni homoni inayozalishwa na kongosho ili kuitayarisha sukari iliyomo kwenye damu kutumika kama chanzo cha nguvu mwilini.

Watu wenye ugonjwa wa kisukari aina ya 2 huwa wana tatizo la sukari iliyo kwenye damu kushindwa kuingia kwenye seli za mwili. Matokeo yake ni viwango vya sukari kwenye damu kuwa juu.

Dalili huweza kujumuisha kukojoa mara kwa mara na kuwa na mkojo mwingi. Watu walioathirika huweza kupungua uzito na kuhisi uchovu na kiu kuliko kawaida.

Ugonjwa wa kisukari aina ya 2 mara nyingi huweza kudhibitiwa kwa lishe nzuri, mazoezi ya mara kwa mara, na dawa za kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu

Kongamano la mwaka huu Kauli mbiu yake ni ugonjwa wa kisukari, Moyo na mishipi ni hatari(Diabetes and Cardiovascular Risk.)

Katika utafiti wa STEPS uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa mgonjwa ya binadamu (NIMR), na Shirika la Afya Duniani, mwaka 2012 uliohusisha wilaya 50 nchini Tanzania, ulionesha kuwa asilimia 9.1 ya Watanzania wenye umri kati ya miaka 25 hadi 64 wana ugonjwa wa kisukari.

Hiyo ilimaanisha kuwa, katika kila watu 11 nchini mtu mmoja ana kisukari.

Mgeni Rasmi katika chakula cha jioni cha kongamano hilo ni waziri Wa afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema "Takwimu zetu za mwaka 2012 zinaonesha kwa kila watu 100 kati ya hao watu tisa wanaugua ugonjwa wa kisukari" 



Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari katika halfa ya chakula cha jioni la kongamano la sita la vipindi maonyesho ya kisayansi. 


"lengo la mkutano huu ni kujadili kwa pamoja jinsi gani kuboresha huduma kwa wagonjwa wa kisukari kwa huu Ukanda wa Afrika Mashariki" alisema Ummy Mwalimu. 

Kwa upande mwingine Waziri Ummy Mwalimu amewashauri watu kafanya mazoezi hata ya kutembea na tupunguze matumizi ya chumvi nyingi, sukari nyingi na mafuta mengi katika chakula ili kuepukana na ugonjwa wa kisukari. 

Pia katika mkutano huo Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania imewakilishwa kiongozi na daktari bingwa ya magonjwa ya kisukari Profesa Kaushik Ramaiya. 



Profesa Kaushik Ramaiya akizungumza katika Mkutano wa sita wa tafiti za kisayansi na maonyesho. 



Profesa Kaushik Ramaiya ni Daktari Mshauri na Msimamizi Msaidizi wa Tiba katika Hospitali ya Shree Hindu Mandal, Dar es Salaam, Tanzania. Dk Ramaiya ana nyadhifa zingine kadhaa za heshima kama vile Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Kisukari, Mhe. Katibu Mkuu wa Chama cha Kisukari Tanzania na Mjumbe wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Wizara ya Afya, Govt. wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na Mjumbe wa Baraza la Madaktari la Tanganyika. Ametoa machapisho mengi kuhusu utafiti wa kisukari na ametekeleza mipango na tafiti nyingi kuweka kisukari kwenye ajenda ya afya barani Afrika. Dk Ramaiya amekuwa chimbuko na mradi unaohusika na miradi kadhaa inayofadhiliwa na WDF nchini Tanzania. Dk Ramaiya ni raia wa Tanzania, mwenye makazi yake jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa kongamano la sita wanasayansi na maonyesho ya sayansi Profesa Kaushik Ramaiya akizungumza na waandishi wa habari katika halfa ya chakula cha jioni. 


Naye Mratibu  mkuu wa kongamano hilo Profesa Kaushik Ramaiya alisema kuwa mkutano huu unachukua kikundi cha waatalam wote kutoka Afrika mashariki tunakaa pamoja na kuangalia hali ya sasa ya ugonjwa yasiyo ambukizi,kuangalia  changamoto na kuangalia uboreshaji wa kinga katika jamii ni kipi cha kufanya ili kuepuka magonjwa hayo. 

"Kama tukizumnguzia changamoto ya kuzuia haya magonjwa watu wasiopenda  kutembea  au kukjmbia hata kwa dakika arobaini tano  kwa siku, kupunguza uvutaji wa sigara,kupunguza   unywaji wa pombe na kuacha  ulaji wa vyakula visofaa ili kuepuka maambukizi ya magonjwa yasiyo ambukizi inatakiwa watu wahamasishwe mara kwa mara" alisema Profesa Kaushik Ramaiya 

"Lengo ya mkutano huu ni kuangalia kwamba katika nchi ya Afrika mashariki kuna tafiti gani zimetokea katika ugonjwa wa kisukari kudhibiti vizuri na magonjwa pamoja na kuangalia magonjwa mengine Yasiyo ambukizi mfano blood pressure, moyo, mifupa, miguu, figo, macho pamoja na stroke"alisema Profesa Kaushik Ramaiya 

Pia Profesa Kaushik Ramaiya amesema kuwa Asilimia themanini (80%) wanaopata ugonjwa wa kisukari ni kutokana na mitindo ya maisha yao kwa wanakosa maisha bora ya kufuatilia afya zao hivyo wanakuwa na Dalili ya type Two diabetes bila ya kujua

Kongamano hili limeshirikisha takribani mataifa ishirini na sita (26) kutoka nchi za Afrika na pamoja na nchi kumi na nne(14) kutoka nje ya Afrika  Uganda, Kenya, Zambia, Zimbabwe, Msumbiji, Nigeria, Ghana,Ethiopia, Ivory Coast, South Afrika, Senegal na kutoka nje Afrika kuna Finland, UK, USA, Singapore, Ujerumani na mataifa mengine mengi. 











Post a Comment

0 Comments