Na Mwandishi wetu Kibaha
Katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukuza na kuinua mchezo wa netiboli mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Selina Koka ametoa vifaa mbali mbali vya mchezo huo kwa wanawake wa kata ya Mbwawa ili waweze kuanzisha timu ya mchezo huo.
Mke wa Mbunge huyo ambaye pia ni mlezi wa Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mji ametoa vifaa hivyo wakati wa ziara la Mwenyekiti Uwt katika kata ya Mbwawa yenye lengo la kuzungumza na wanachama pamoja na kukiimarisha chama.
Selina alisema anatambua Kuna wanawake wengi wenye vipaji ndio maana akaamua kutoa sapoti ya kuchangia vifaa hivyo kwa ajili ya kukuza mchezo wa netiboli hususan kwa wanawake wa Jimbo la Kibaha.
"Natambua kwamba tupo katika ziara hii ya UWT lakini mm katika kuendeleza sekta ya michezo nimeona ni vizuri kutoa vifaa hivi kwa wanawake wa ccm kata ya CCM ili wawze kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa netiboli,"alisema Selina.
Alisema kwamba amepania kuanzisha ligi ya mpira wa kikapu katika kata mbali mbali na kwa kuanzia ametoa jezi 14 pamoja mpira kwa ajili ya kuanzisha timu ya mchezo wa netiboli kwa wanawake wa kata ya Mbwawa.
Katika hatua nyingine alitoa wito kwa wanawake wanafanya mazoezi na kuanzisha timu za mpira wa netiboli na kuahidi kuendelea kushirikiana nao bega kwa bega katika kuukuza mchezo huo.
Kwa upende wake Mwenyekiti wa Juimuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Elina Mgonja alimpongeza Selina Koka kwa kuona umuhimu wa kukuza mchezo wa netiboli pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa wanawake hao.
Nao baadhi ya wanawake wa chama cha mapinduzi ambao wamepatiwa vifaa hivyo vya michezo wameahidi kuvitunza pamoja na kuunda timu ya kata ya mchezo wa netiboli ili kuweza kulete mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika mchezo huo.
0 Comments