Na mwandishi wetu
Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 lina jumla ya Vijiji 68 na Vitongoji 374.
Jimbo hili lina Sekondari 28, kati ya hizo 26 ni za Kata/Serikali na 2 ni za Binafsi (private). Wanavijiji wanajenga sekondari nyingine 10.
*Nyanja Sekondari: miundombinu ya elimu:*
Sekondari hii ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vya Bugunda, Bwasi na Kome. Ilifunguliwa Mwaka 2006, ina wanafunzi 495 na walimu 11.
Sekondari hii haina maabara hata moja, haina jengo la utawala na ina upungufu wa vyumba vinne vya madarasa. Kuna nyumba moja tu ya walimu.
*Maabara 3 kujengwa ndani ya miezi 4:*
Kikao kilichohudhuriwa na baadhi ya wanavijiji, viongozi wa Chama na Serikali wa Kata ya Bwasi na Mbunge wa Jimbo kiliazimia kwamba ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (physics, chemistry and biology) uanze mara moja na maboma yawe yamekamilika ifikapo tarehe 15.8.2024.
Mbunge wa Jimbo atarudi shuleni hapo kukagua ujenzi huo.
*Upatikanaji wa vifaa vya ujenzi:*
Harambee ya Mbunge wa Jimbo iliyopigwa Septemba 2023 iliwezesha kupatikana kwa:
*Saruji Mifuko 41 kutoka kwa wananchi
*Tsh 549,000
*Saruji Mifuko 100 za Mbunge wa Jimbo.
Hata hivyo ujenzi haujaanza kwa sababu mbalimbali ambazo ziko mikononi mwa Serikali ya Kata na vijiji vyake vitatu!
*Mchango wa Mfuko wa Jimbo:*
Saruji Mifuko 100 imegawiwa kwenye shule hii.
*Michango kutoka kwa Wana-Bwasi na Wadau wengine wa Maendeleo:*
*Michango ya vifaa vya ujenzi ipelekwe kwa Mkuu wa Shule
*Michango ya fedha ipelekwe moja kwa moja kwenye Akaunti ya Shule ambayo ni:
Benki: NMB
Akaunti Na: 30301200349
Jina: Nyanja Sekondari
*WANA-BWASI TUJITOKEZE KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU YA SEKONDARI YA KATA YETU*
*Picha za hapa zinaonesha:*
Mbunge wa Jimbo akikabidhi saruji ya ujenzi wa maabara tatu (3) za masomo ya sayansi ya Nyanja Sekondari ya Kata ya Bwasi.
Wananchi wakiwa wamegawiwa vitabu viwili viwili (Volumes III&IV) vinavyoelezea mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo letu.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz
P. O. Box 6
Musoma
Tarehe:
Alhamisi, 11.4.2024
0 Comments