VIJANA GEITA WAMUOMBA M/KITI UVCCM MKOA WA GEITA KUPELEKA KILIO CHA ASILIMIA 10

 




Na mwandishi wetu
 

Vijana waishio  Halmashauri ya Mji wa Geita wamemuomba Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM),Mkoa wa Geita,Manjale Magambo kufikisha kilio chao serikali cha kupatiwa asilimia 10 ya mkopo kutoka Serikalini.

Mikopo ya asilimia 10 ilikuwa ikitolewa kwenye Makundi maalumu ya Vijana, Wanawake na Walemavu kupitia Halmashauri zote zilizopo Nchini, ilisitishwa Mwaka 2023 wakati Waziri Mkuu akihitimisha hoja ya makadilio ya maombi na matumizi ya fedha kwa mwaka 2023/24.

Kufuatia kusimamishwa mikopo hiyo kwa muda mrefu sasa baadhi ya vijana mjini Geita wakiwa kwenye kijiwe cha kahawa maarufu kwa jina la Mlumba wamehoji ni lini serikali itaachia mikopo hiyo ambayo ilikuwa na msaada wa wao kujikwamua kiuchumi.
 
“Mhe Mwenyekiti wetu wa vijana sisi  kama vijana wenzako tunalizishwa na namna ambavyo umekuwa mstari wa mbele kutetea masrahi yetu kama vijana lakini kusimamishwa kwa mikopo ya asilimia 10 kwetu limekuwa ni tatizo kubwa mfano sisi bodaboda tulikuwa tunakopeshwa kipindi kile na kufanya marejesho kwa wakati lakini sasa hivi tangu mikopo iliposimamishwa tumekuwa na uwitaji tunaomba suala hili tusaidia kufikisha kilio chetu”Rashid Juma Mwendesha Boda boda.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita Manjale Magambo amewatoa hofu vijana na kusema serikali iko kwenye mchakato wa kuirudisha mikopo hiyo.


“Mnajua vijana wenzangu kwamba Bunge kwasasa linaendelea niwaondoe wasi wasi mikopo inarudi serikali ilisimamisha ni kutokana na urasimu uliokuwepo lakini kupitia Bunge la Bajeti mikopo inaenda kurudi cha kuwashauli hakikisheni mnaunda vikundi ambavyo vitawasaidia kupata mikopo”Manjale Magambo,M/kiti wa UVCCM Mkoa wa Geita..

Pamoja na mambo mengine Manjale  Magambo amekabidhi tv na king’amuzi kwa nia ya wananchi kufuatilia matukio mbalimbali huku akitoa ahadi ya kukikarabati kijiwe cha kawaha cha Mulumba ambacho kimejipatia umaarufu kutokana na viongozi mbalimbali wa Kitaifa kukitembelea na kupata maoni ya wananchi kuhusu mustakabali wa maendeleo ya nchi.



Post a Comment

0 Comments