RAIS MWINYI AIPONGEZA BENKI YA STANBIC KUFUNGUA TAWI ZANZIBAR

 


Na mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amepongeza uamuzi wa Benki ya Stanbinc Tanzania wa kuwa na Tawi Zanzibar  kwani kutaongeza  idadi ya Benki na kurahisisha huduma kwa wananchi.

Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Uongozi wa  Benki ya  Stanbic Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa  Bodi ya Benki hiyo Patrick Rutabanzikwa waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 13 Novemba 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa ukuaji wa kasi wa Uchumi unaoendelea hivi sasa unahitaji kuwepo na mchango wa taasisi  makini za kifedha .

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Benki hiyo Patrick Rutabanzikwa ameeleza kuwa maendeleo yanayoonekana Zanzibar hivi sasa na ongezeko la  mahitaji ya taasisi za kibenki kwa wananchi kumechochea kwa Stanbic kufungua Tawi lake.

Benki ya Stanbic  itajenga Tawi hilo katika Mtaa wa Biashara wa Mlandege na inatarajia kutumia kiasi cha Shillingi Milioni Mia nane kukamilisha Ujenzi huo.









Post a Comment

0 Comments