Na mwandishi wetu
Mbunge wa viti maalumu, Lucy Sabu ameihoji Serikali kupitia Wizara ya Afya juu ya mpango wake katika kuwasaidia vijana wanaopata tatizo la afya ya akili kutokana na kukosa ajira.
Akijibu swali hilo bungeni Jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema matatizo hayo yanaweza kukabiliwa kwa kuelimishana namna sahihi ya kufikiria na kuyatazama maisha, na ndio maana Serikali imekuja na mtaala mpya wa elimu ambao utamuandaa mtoto tokea anasoma chekechea kutambua kwamba hata usipoajiriwa maisha yanaweza kwenda.
0 Comments