SHAMIRA ACHANGIA UJENZI NYUMBA YA MTUMISHI MKOA WA KUSINI PEMBA.

 


Na mwandishi wetu

 Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa Zanzibar kwenye muendelezo wa ziara yake amefanya zoezi la ukaguzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa wa Kusini Pemba.

Akiwa katika kikao hiko cha ndani Mshangama alisisitiza viongozi vijana kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo ya Jumuiya na malengo ya CCM ya kuendelea kushika dola, huku akikumbusha viongozi vijana kujiimarisha kuja kuwa viongozi wakubwa wa baadaye katika Chama na serikali. 

Mshangama amekabidhi shilingi milioni moja kwa lengo la kuchangia ujenzi wa nyumba ya Katibu.
Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.




Post a Comment

0 Comments