Na mwandishi wetu
Viongozi mbalimbali wa kitaifa na wageni waalikwa leo tarehe 10 Agosti 2025 wamewasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kushiriki ibada maalum ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Job Yustino Ndugai.
Ibada hiyo, inayofanyika kwa heshima ya mchango mkubwa wa Hayati Ndugai katika uongozi na maendeleo ya taifa, inatarajiwa kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye atakuwa miongoni mwa viongozi wakuu watakaotoa heshima za mwisho.
Viongozi wa Serikali, Wabunge, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, ndugu, jamaa na wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kushiriki tukio hilo la kumbukizi.
Hayati Job Yustino Ndugai alihudumu kama Spika wa Bunge la 11 kuanzia mwaka 2015 hadi 2022, na anabaki kukumbukwa kwa msimamo, nidhamu na mchango wake katika kuimarisha shughuli za Bunge na ustawi wa demokrasia nchini
0 Comments