Mbeto: NaneNane 2025 Rais Samia tembea kifua mbele

 



Na Mwandishi Wetu, Zanzibar 


Chama cha Mapinduzi  kimesifu juhudi na umakini wa  serikali ya Rais Dk  Samia  Suluhu  Hassan kwa  kuliingizia Taifa  trilioni 9.21 Mwaka 2025 kutoka Trilioni 3.12  Mwaka 2020  kwa  mauzo ya Mazao Nje.

CCM kimejigamba kwa kuifanya   sekta ya kilimo  kufikia lengo  hilo na juhudi za  serikali kwa kukifanya   kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC  Zanzibar ,Idara ya Itikadi  ,Uenezi  na Mafunzo , Khamis Mbeto  Khams,  aliyesema Serikali  ya Awamu ya sita imetimiza wajibu wake kwa vitendo nchini .  

Mbeto alisema hatua ya kupanda  mauzo ya mazao ya kilimo nje ,  yameongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2019|2020 sawa na kufikia  trilioni 3.12 hadi Dola za Marekani bilioni 3.54 sawa na 9.205 Trilioni  Mwaka 2023|2024

 Alisema ongezeko hilo linaonyesha mkakati kabambe  wa  serikali  katika kuimarisha  kilimo kupitia uwekezaji kwa miundombinu ya umwagiliaji, utafiti, pembejeo bora na upanuzi wa masoko ya nje.

"Tunaposema Serikali ya Awamu ya sita  imechapakazi huwa  tunamaanisha si  domo mtindi.  Sekta ya kilimo imeimarika kutoka asilimia 2.6 mwaka 2021 hadi  kufikia asilimia 4.2 mwaka 2023 "Alisema Mbeto. 

Aidha  , aliutaja ufanisi huo umetokana na mikakati ya kisera na utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya kilimo na ukuaji unaotarajiwa  kuongezeka hadi  kufikia asilimia 5  mwaka 2025.

"Kilimo kinatarajia kukua hadi kufikia asilimia 10 mwaka 2030

Ikiwa ni  sehemu ya malengo ya muda mrefu ya  Serikali na kukua kwa  Uchumi kupitia Mapinduzi ya kilimo" Alieleza  .

Mbeto  akizumgumzia  uzalishaji wa zao la  korosho,  alisema Tanzania imekuwa kinara wa uzalishaji katika ukanda wa  Afrika ya Mashariki.

'Katika Awamu ya sita korosho uzalishaji  umepata msukumo  katika na ongezeko   kutoka tani  210,786 msimu wa 2020|2021 hadi kufikia 528,263.82 msimu wa 2024|2025, sawa  ongezeko la  asilimia 150.61" Alisema  

Katibu huyo Mwenezi  alitaja ongezeko hilo linaifanya Tanzania kuongoza kwa  uzalishaji wa  korosho Afrika Mashariki na kuwa ya pili  barani Afrika huku  ikiwa  ya Tano duniani.

" Mafanikio haya yamatokana na juhudi za Serikali katika kuongeza upatikanaji wa pembejeo bora na  huduma za ugani. Serikali imewawezesha Wakulima kupitia mifumo ya Ushirika na Masoko ya uhakika" Alisisitiza Mbeto .

Post a Comment

0 Comments