RC CHALAMILA ATEMBELEA NA KUKAGUA MABANDA YA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MASHARIKI

 




-Afurahishwa na ushiriki mkubwa pamoja na maandalizi mazuri ya maonesho hayo 


-Asema Rais Dkt Samia kupitia Wizara ya kilimo ameongeza bajeti kubwa kuliko wakati mwingine wowote


-Asisitiza Sera nzuri ni matokeo ya uongozi mzuri atoa wito " Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi"

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila Agosti 6, 2025 ametembelea na kukagua mabanda mbalimbali ya maonesho kanda ya mashariki Mkoani Morogoro.

Akikagua mabanda ya maonesho ya NANENANE RC Chalamila amefurahishwa na ushiriki mkubwa wa wakulima, wavuvi na wafugaji, Taasisi, Halmashauri, pamoja na  makampuni mbalimbali katika maonesho hayo.

Aidha RC Chalamila amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya Kilimo ameongeza bajeti kubwa kuliko nyakati nyingine yoyote hivyo tuna kila sababu ya kumshukiru Mhe Rais.

Vilevile RC Chalamila amesema mwaka huu tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu, sera nzuri ni matokeo ya uongozi bora kila mmoja wetu amuamasishe mwingine kushiriki uchaguzi mkuu kama kauli mbiu inavyosema "Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi"

Mwisho Maonesho ya NANENANE Kanda ya Mashariki yanajumuisha Mikoa minne, Dar es Salaam, Morogoro, Pwani na Tanga, kwa mwaka huu 2025 kikaifa maonesho hayo yanafanyika Mkoani Dodoma.











Post a Comment

0 Comments