RC MALIMA AWAKARIBISHA WANANCHI KUSHIRIKI "SELOUS MARATHON 2025" MOROGORO

 



Na mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amewakaribisha wadau wa michezo na wananchi wote waliojisajili kushiriki mbio za "Selous Marathon 2025" zinazotarajiwa kufanyika mkoani humo Agosti 23, mwaka huu.

Akizungumza Agosti 20, alipokutana na waandaaji wa mashindano hayo, Mhe. Malima amesema mbio hizo zitatumika na wananchi wa rika mbalimbali na zitakuwa na umbali wa kilomita 5, 15, na 21.

Mhe. Malima ameongeza kuwa mashindano haya hayatahitaji tu mshikamano wa kijamii, bali pia yatahamasisha watalii kutembelea vivutio mbalimbali vya mkoa wa Morogoro, jambo litakalosaidia kukuza uchumi na kuongeza mapato ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Aidha, amewataka wananchi kushiriki kwa wingi, huku akiwakaribisha pia wageni kutoka maeneo mbalimbali, kwa lengo la kuboresha afya za watu binafsi na kuimarisha mshikamano na udugu ndani ya jamii.

Pia, Mhe. Malima ameeleza kuwa mchezo huu utatoa fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara wadogo na wakubwa na kuutangaza Mkoa wa Morogoro kama kitovu cha utalii na michezo nchini.

Post a Comment

0 Comments