Ummy Mwalimu Awashukuru WanaTanga, Ampongeza Kassim Makubel Kwa Kuteuliwa Kugombea Ubunge CCM Tanga Mjini

 



Nimepokea uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa moyo wa shukrani. Quran Tukufu inatufundisha kuwa Allah ndie mpangaji na ni bora kwetu. ALHAMDULILLAH

Ndugu zangu wanaTanga Mjini, nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuniamini kuwa Mbunge wenu kwa kipindi cha miaka 5 (2020 - 2025) Nafurahi kuona kuwa utumishi wangu kwenu umewagusa wengi na umeacha alama kubwa za kimaendeleo katika Jimbo letu. Asanteni kwa ushirikiano mzuri mlionipatia ktk kipindi chote cha Utumishi wangu.

Kwa dhati ya moyo wangu, ninawashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Tanga kwa kunipa kura nyingi ktk mchakato wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo letu Tanga Mjini kwa kipindi cha 2025 - 2030. Mlinikopesha imani kubwa sana Nitaienzi na kuithamini imani hii daima. 

UAMUZI wa vikao vya Chama ni lazima UHESHIMIWE. Nampongeza Ndugu Kassim Amar Mbaraka (Makubel) kwa kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM Tanga Mjini. 

Ninawaomba wanakimji wenzangu hususani wanaCCM tumpokee na tumpe ushirikiano ili kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa Rais Dkt Samia, Mbunge Kassim Makubel na Madiwani katika kata zote 27 za Jimbo la Tanga Mjini

Mwisho, ninawashukuru wote kwa salaam za heri, sala na dua zenu kwangu. Nimeuona upendo wenu. Asanteni sana. Allah ni Mkarimu. 


Ndugu yenu,

Ummy Mwalimu

#OdoUmmy

#OktobaTunatiki✅✅✅

Post a Comment

0 Comments