WAKULIMA MKINGA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA KILIMO BORA CHA MWANI

 




Na.Mwandishi Wetu –Tanga


Vikundi zaidi ya ishirini na Sita Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga vimejengewa uwezo juu ya kilimo bora, utunzaji kumbukumbu, kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao pamoja na masoko ya zao la mwani.

Vikundi hivyo vya wakulima vinahushisha wanawake, vijana na wazee wanaojihusisha na kilimo cha zao la mwani Wilaya ya Mking. 

Mafunzo hayo yanafanyika kwa nadharia na vitendo ambapo wanavikundi wameweza kupata ujuzi kwa nadharia kisha mafunzo elekezi kwa vitendo ya namna ya kulima kwa ubora zao hilo.

Mafunzo hayo yanayofadhiriwa na Serikali ya Japan pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini,Tawi la Mwanza kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu kwa lengo la kuwafikiwa wakulima wa zao la Mwani ili kuinua vipato vyao na kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.








Post a Comment

0 Comments