KYERWA MITANO TENA KWA DKT. SAMIA NI SUALA LA MUDA TU

 



Kyerwa, Kagera – Septemba 7, 2025

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi, ameendelea na mikutano yake ya kampeni na kupata kibali kikubwa kutoka kwa wananchi wa Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera.

Maelfu ya wananchi waliojitokeza kumpokea Dkt. Nchimbi wamesisitiza kuwa CCM ndiyo chaguo sahihi, wakiahidi kurundika kura za kishindo ifikapo tarehe 29 Oktoba 2025.

Akizungumza na wananchi, Dkt. Nchimbi aliwashukuru wakazi wa Kyerwa kwa mapokezi makubwa na kwa imani   waliyoonesha kwa CCM, akiwataka kudumisha mshikamanio na mshangao wa kijani kuelekea ushindi wa kishindo.

Wananchi walioshiriki mkutano huo walisema kuwa sera na utekelezaji wa CCM chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan umewaletea maendeleo makubwa, na hivyo "mitano tena" ni suala la muda tu.


#GreenArmyOktobaTunatiki✅
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#RundikaKuraKwaDktSamia2025

 

Post a Comment

0 Comments