MWALIMU PAWA AONGOZA WANAFUNZI WA KAZITA KATIKA ZIARA YA MAFUNZO MAPANGO YA AMBONI TANGA

 




Tanga | 07 Septemba 2025

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kazita, Wilayani Muheza, mkoani Tanga, wakiongozwa na Mwalimu Jao Kalesi maarufu kama Mwl. Pawa, wamefanya ziara ya mafunzo ya vitendo katika Mapango ya Amboni Tanga, kisiwa kinachojulikana kwa historia yake ya utamaduni na harakati za kupigania uhuru nchini.

Ziara hiyo imelenga kuwapa wanafunzi nafasi ya kujifunza vitendo kuhusu historia, urithi wa utamaduni, utunzaji wa mazingira na shughuli za utalii.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Huduma za Utalii na Masoko (NCAA), Mariam Kobelo, aliwashukuru walimu na wanafunzi kwa juhudi za kuendeleza elimu ya uhifadhi na kuwataka kuwa mabalozi wazuri wa Mapango ya Amboni. Pia alimpongeza Mwl. Kalesi kwa kutumia nyimbo na muziki, hususan wimbo maarufu wa Mbosso “Pawa”, kufundisha na kuhamasisha wanafunzi kujifunza kwa ari.

Afisa Uhifadhi Daraja la Pili na Mkuu wa Mapango ya Amboni, Ramadhan Rashid, alieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025, Mapango ya Amboni yalipokea wageni 19,743 na mapato ya zaidi ya Shilingi milioni 40, akionyesha mchango mkubwa wa mapango haya katika maendeleo ya Taifa kupitia utalii.





Post a Comment

0 Comments