Wafanyabiashara wa Oman Watembelea Mkoa wa Pwani Kujionea Shughuli za Viwanda na Biashara

 




📍 Pwani, Tanzania – Septemba 7, 2025

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka Oman umetembelea Mkoa wa Pwani kwa lengo la kujionea shughuli za viwanda na biashara pamoja na kuangazia fursa za uwekezaji kati ya Tanzania na Oman katika sekta mbalimbali.

Ujumbe huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara na Viwanda Mkoa wa Al Wusta na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Chama cha Biashara na Viwanda cha Oman, Dkt. Salem Al-Junaibi(Mb)

Katika ziara yao mkoani humo, walitembelea Kiwanda cha Nyama cha Union Meat kilichopo Kibaha, ambapo walishuhudia uzalishaji wa nyama na kujadili uwezekano wa kushirikiana katika sekta ya kilimo na ufugaji, hususan bidhaa za viwandani kama nyama.

Aidha, wafanyabiashara hao walitembelea Eneo la Viwanda la KAMAKA na kushuhudia maendeleo ya miundombinu pamoja na jitihada za Serikali za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Kesho, tarehe 8 Septemba 2025, ujumbe huo unatarajiwa kutembelea makao makuu ya TCCIA na kusaini Mkataba wa Ushirikiano kati ya TCCIA ya Tanzania na Oman. Baada ya hapo, watashiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji utakaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki kutoka sekta ya umma na binafsi wanatarajiwa kushiriki.


📌 Ziara hii ni sehemu ya jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Oman, ikilenga kuleta tija katika sekta za viwanda, kilimo na uwekezaji.















Post a Comment

0 Comments