HALMASHAURI ZOTE DAR, ZATAKIWA KUTUMIA JESHI LA AKIBA.

 



Na mwandishi wetu

MKUU wa Wilaya  ya Temeke, Mhe Sixtus Mapunda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, amezielekeza Halmashauri ya Jiji  na Manispaa zote Mkoani humo kuhakikisha zinawatumia kikamilifu  wahitimu wa mafunzo ya awali ya Jeshi la Akiba katika utekelezaji wa operesheni mbalimbali.

Ametoa maelekezo hayo leo Agosti 15, 2025 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe  Albert Chalamila, katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Awali ya Jeshi la Akiba  Kundi  la 63/2025 yaliyofanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi la Wanamnchi Tanzania ya  Twalipo, wilayani Temeke.

“Halmashauri zote katika shughuli zao na operesheni zao ziwatumie  vijana hawa, Wakurugenzi muwatumie wahitimu hawa  haraka kabla hawajarudi mtaani,” amebainisha  Mapunda ambapo amesema  vijana hao wakiachwa  mtaani kwa kipindi kirefu  bila kutumika  watasahau kwa haraka kiapo chao.

“Tuna operesheniu za kukusanya mapato. Tuna maandalizi ya uchaguzi mkuu na kusimamia taratibu mbalimbali katika Halmashauri zetu. 

"Hawa vijana  wako tayari kutumika,”ameeleza Mapunda.

Aidha, ametoa  wito kwa wahitimu hao  kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu  unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu pia ametoa rai siku ya uchaguzi mkuu kujitokeza kwa wingi kupiga kura, "ninawakabidhi jukumu la kwenda  kuhamasisha vijana wenzenu kujitokeza kupiga kura,” amesema Mapunda 

Vilevile amewataka, wahitimu hao kuishi kiapo walicho apa na kujiepusha kutumia mafunzo waliyopata  katika vitendo viovu.

Kwa upande wa Mshauri wa Jeshi la Akiba Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Emmanuel Kasyupa, alisema mafunzo hayo  yalijumuisha vijana kutoka wilaya tano za Mkoa huo ambazo ni Ilala, Temeke, Kinondoni, Kigamboni na Ubungo, mafunzo  yalianza April nne mwaka huu yakiwa na wanafunzi 414. wanafunzi 66 walishindwa kuendelea kutokana na sababu  mbalimbali zikiwemo za utoro, matatizo ya afya na utovu wa nidhamu aidha jumla ya wahitimu wote ni 348, wanaume  263  na wasichana 85 ambapo mafunzo hayo yalifanyika kwa wiki 18.

Hata hivyo Kanali Kasyupa amebainisha, wakufunzi wa mafunzo hayo walitoka katika Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Usalama wa Taifa na  Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

 “Kiapo kimesikika Mmeahidi kuwa watiifu na waaminifu  kwa Amiri Jeshi Mkuu  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mtakuwa watiifu kwa raia . msiende kukiweka  kiapo hiki katika begi ikiwezekana bandikeni sebuleni ili mgeni akija atambue unawajibu gani kwa Taifa,”.

Sambamba na hilo amesisitiza  wahitimu hao  kulinda  uhuru na uchumi  wa Nchi kama walivyo apa.

kwa kuwa Askari hao wamefikia kiwango kinachokubarika  katika Jeshi la akiba na wapo tayari kutumikia  taifa katika kutekeleza majukumu mbalimbali.

Ifahamike kuwa katika mafunzo hayo wahitimu hao walipata masomo mbalimbali kwa nadharia  na vitendo, ikiwa ni pamoja na kwata, ukakamavu, mbinu za kivita, ujanja wa porini, usomaji ramani, huduma ya kwanza, zimamoto, uhamiaji, usalama wa taifa, kuzuia na kupambana na rushwa , silaha ndogondogo, utimamu wa mwili, uraia, kazi za polisi, ,Sheria za Jeshi la Akiba, na vita vya  msituni.

Mwisho, katika risala yao  wahitimu hao waliiomba Serikali kuongeza bajeti ya mafunzo ya jeshi la akiba na kuwapa kipaumbele  kujiunga na JKT  na  taasisi zingine za Serikali.




Post a Comment

0 Comments