MWANAMKE INITIATIVES FOUNDATION (MIF) YATOA UFADHILI KWA KIKUNDI UFUNDI CHA NGUVU MOJA

 


Na mwandishi wetu

Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF), chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, tarehe 12 Agosti, 2025 imeendelea kutimiza adhma yake ya kutoa ufadhili kwa makundi mbalimbali hususan kwenye miradi ya sekta ya elimu Makunduchi, Zanzibar. 

Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) kupitia Mradi wa Elimu ya Ufundi, iliunga mkono juhudi za Kikundi cha Vijana Wajasiriamali kwa kuwapatia Mashine (Vyerehani) za kushonea nguo kama mtaji wa kuanzia pamoja na kuwalipia pango la sehemu watakayokuwa wanashona. 

Kikundi hiki cha ujasiriamali kiitwacho NGUVU MOJA, kilidhaminiwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), wakati wanapata mafunzo ya stadi za ufundi katika Chuo cha Ufundi (VTA ) kilichopo Makunduchi, Zanzibar. 

Aidha, Siku hiyo hiyo, kupitia mpango wa Kuimarisha Vyuo vya Ufundi, Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) iligawa Magodoro 200 kusaidia vijana wa chuo cha Mafunzo ya Amali - Makunduchi, ili kuhakikisha wanapata mapumziko bora na kuweza kuzingatia kikamilifu masomo yao.

Uongozi wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) umesema kuwa umejizatiti kuwawezesha vijana kufungua uwezo wao. Ungana nasi katika kuunda fursa na kubadilisha mustakabali wa vijana!

Post a Comment

0 Comments