Na mwandishi wetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, Bi. Regina Bieda, kwa niaba ya Halmashauri, amesaini mkataba wa mauziano ya ardhi yenye ukubwa wa ekari 625 iliyopo Kwala, kwa ajili ya uwekezaji, na Mwenyekiti wa Kampuni ya Sino Dar.
Hafla ya utiaji saini huo imefanyika sambamba na uzinduzi wa Taasisi ya TISEZA (Tanzania Special Economic Zones Authority), taasisi mpya iliyoundwa baada ya kuunganishwa kwa EPZA (Export Processing Zones Authority) na TIC (Tanzania Investment Centre).
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, ambaye alisisitiza kuwa uwekezaji huo utachochea kasi ya ukuaji wa uchumi, kuongeza ajira, na kuimarisha hadhi ya Kwala kama kitovu cha biashara na usafirishaji.
Uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza thamani ya kiuchumi wa Mkoa wa Pwani na kuimarisha nafasi ya Kibaha kama eneo la kimkakati kwa uwekezaji mkubwa nchini.
0 Comments